Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa kikao hicho kimesimamiwa na Kituo cha Utafiti na Uchunguzi wa Masuala ya Wanawame cha Taasisi ya Ulaya ya Sayansi za Kijamii mjini Paris.
Kikao hicho kimejadili na kuchunguza baadhi ya masuala yanayohusiana na haki za mwanamke katika ndoa.
Masuala mengine yaliyochunguzwa ni pamoja na vigezo vya sheria za Kiislamu katika masuala ya ndoa, haki za mwanamke za kuweka masharti wakati wa kufunga ndoa na kutoa talaka, hisa ya mwanamke katika mali ya mume na kadhalika. 748306