Mashindano hayo ya Qur'ani yaliyoandaliwa na Madrasa ya Irfania yalikuwa na washiriki 25 kutoka majimbo kadhaa ya India kama vile Gujarat, Maharashtra, Bengal, Tamil Nadu, Bihar na jimbo mwenyeji Uttar Pradesh.
Mashindano hayo yalikamilika kwa kuzawadiwa maqari watatu ambao kwa mujibu wa rai ya jopo la majaji ndio waliokuwa wasomaji bora. Aidha walitunukiwa shahada za heshima na bodi ya utendaji ya mashindano hayo.
748898