Sayyid Hamed Malakuti Tabar, Mwambata wa Utamaduni wa Iran huko Sudan amekutana na Suleiman Othman Mkuu wa Chuo Kikuu cha Qur'ani nchini humo na wameafikiana kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika masuala ya Qur'ani.
Ustadh Othman ameashiria historia ya Chuo Kikuu cha Qur'ani nchini Sudan na kusema mwaka 1991 chuo hicho kilipandishwa cheo na kuwa chuo kikuu na sasa ni kati ya vyuo vikuu vitano vya juu nchini Sudan.
"Kuna uhusiano mzuri wa kidini na kiutamaduni kati ya Iran na Sudan", amesema na kuongeza kuwa amashatembelea Iran mara tano kuhudhuria vikao vya kidini na kielimu.
Ustadh Suleiman Othman ameutaja ustaarabu na utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa muhimu na kuongeza kuwa uwezo mkubwa wa Iran ni chanzo cha heshima kwa umma wa Kiislamu duniani.
Naye Sayyid Hamed Malakuti Tabar amefafanua mbinu za kufunza Qur'ani katika vyuo vikuu vya Iran na kusema uhusiano wa vyuo vikuu vya nchi mbili ni wa kiwango cha juu.
748261