Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Qur'ani Tukufu katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu mjini New Delhi, Maulana Furqan Qassimi amesema kuwa nchi za kibeberu zinapanga njama za kuharibu na kutokomeza dini ya Kiislamu na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini kwamba mfumo huo unaotegemea azma ya kitaifa na misingi ya thamani za Mapinduzi ya Kiislamu utaendelea kuwa imara na kufuatilia malengo ya ustawi na maendeleo katika nyanja zote. Ameongeza kuwa hii leo mwamko wa Kiislamu onaonekana wazi katika taifa la Iran na kwamba athari zake zimeenea katika nchi nyingine za Kiislamu.
Mwanafikra huyo wa Kiislamu wa India amesema kwamba Iran inayachukulia mafundisho ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu kuwa msingi madhubuti na pia ufunguo wa kutatuliwa matatizo yote ya mwanadamu.
Amesema kwa kutegemea msingi huo, taifa la Iran limefanikiwa kufikia ushindi mkubwa na kusimama kidete mbele ya madola ya kibeberu. 749836