IQNA

Msomi wa Misri akosoa misimamo ya maulamaa kuhusu hali ya nchi hiyo

16:45 - February 19, 2011
Habari ID: 2083413
Mwanafikra wa Misri Kamal al Halbawi ambaye pia ni mwanachama wa ngazi za juu wa chama cha Ikhwanul Muslimin amekosoa misimamo ya baadhi ya maulamaa kuhusu mabadiliko na hali ya mambo ya Misri.
Kamal al Halbawi ambaye alikuwa akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu mjini Tehran amekosoa misimamo ya baadhi ya maulamaa kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini Misri na kusisitiza kuwa misimamo yao ya kumuunga mkono dikteta aliyeng'olewa madakani nchini humo Hosni Mubarak inapingana na mafundisho ya Qur'ani na ubinadamu.
Amesema siasa za Hosni Mubaraka dhidi ya wananchi wa Palestina zilikuwa za kidhalimu na kwamba katika miaka ya huko nyuma Misri ilikuwa kituo cha harakati nyingi za Kiislamu lakini ilipoteza nafasi hiyo kutokana na kutokuwa na uongozi mzuri uliokuwa kibaraka wa Marekani na Israel.
Al Halbawi ameeleza nafasi ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri na kusisitiza kuwa Wamisri wanataka Rais shujaa kama Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye misimamo na hotuba anazotoa Tehran ndizo hizo hizo anazozitoa mjini New York, Marekani. 750460
captcha