Majlisi hiyo itasimamiwa na Kamati ya Anwarul Qur'ani ya mji wa Saihat kwa mnasaba wa sherehe ya Maulidi ya Mtume Muhammad (saw) na mjukuu wake Imam Ja'far Swadiq (as).
Majlisi hiyo ya kiraa ya Qur'ani itahudhuriwa pia na watu mashuhuri wa kidini na kijamii na viongozi wa taasisi na jumuiya zinazojihusisha na masuala ya Qur'ani katika nchi za kandokando ya Ghuba ya Uajemi.
Kamati ya Anwarul Qur'ani ni taasisi inayojishughulisha na masuala ya kutoa elimu ya Qur'ani na tajwidi katika mji wa Saihat. 750068