Hujjatul Islam Mujtaba Husseini mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Syria amesema kuwa, sambamba na Wiki ya Umoja baina ya Kiislamu, Maulamaa wa Kishia na Kisuni watakutana Damascus kujadili matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa, “Kikao cha nane kitajadili upotofu na shaka kuhusu umoja wa Waislamu na washiriki watajaribu kuwasilisha mapendekezo ya kusuluhisha matatizo yaliyopo”.
Akiashiria warsha zilizotangulia, amesema kuwa, ‘njama za maadui za kuvuruga umoja wa Mashia na Masuni na njia za kukabiliana na njama hizo ni kati ya mambo yaliyojadiliwa katika vikao vilivyopita’.
749707