IQNA

Mkutano wa 24 wa Umoja wa Kiislamu wamalizika mjini Tehran

12:50 - February 22, 2011
Habari ID: 2084343
Mkutano wa 24 cha Umoja wa Kiislamu ulimalizika jana usiku hapa mjini Tehran na kufungwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran, Sayyid Muhammad Husseini.
Katika hotuba yake ya kufunga mkutano huo, Sayyid Husseini amesema kwamba kuna haja ya kudumishwa mshikamano kati ya Waislamu kwa ajili ya kuundwa umma mmoja wenye nguvu katika jamii za Kiislamu.
Ameongeza kwamba, kama hivi sasa tunashuhudia nembo za ukafiri na shirki zinaanguka moja baada ya nyingine katika kipindi hiki cha Mfunguo Sita cha maadhamisho ya maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW basi tukumbuke pia kuwa wakati alipozaliwa Bwana Mtume moto wa dola la Kifarsi ulizima, na hii ni ishara njema kwa wanaadamu waliochoshwa na dhulma, kunyongeshwa na ukandamizaji.
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran ameongeza kuwa, Mkutano wa 24 wa Umoja wa Kiislamu umeshirikisha wanachuoni na wasomi wa Kiislamu kutoka nchi 57 tofauti duniani na jambo hilo limetoa sura bora kabisa ya mshikamano katika safu za Waislamu.
captcha