IQNA

Benki ya Kiislamu ya Dubai kufadhili mashindano ya Qur'ani ya Ras al- Khaimah

11:27 - February 23, 2011
Habari ID: 2085204
Benki ya Kiislamu ya Dubai DIB imetangaza kwamba mwaka huu pia itadhamini mashindano ya Qur'ani ya Ras al-Khaimah.
Kwa mujibu wa tovuti ya ameinfo, huu utakuwa mwaka wa kumi kwa benki hiyo kudhamini mashindano hayo ambayo ni moja ya ratiba muhimu za kila mwaka za Qur'ani katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Moja ya malengo muhimu ya mashindano hayo ni kushukuru na kuwaenzi mahufadhi mashuhuri wa Qur'ani Tukufu, shakhsia wa Kiislamu na taasisi za kielimu na Kiislamu.
Swalah al-Hashimi mmoja wa maafisa wa benki ya DIB amesema kuhusiana na suala hilo kwamba uungaji mkono wa benki hiyo kwa shughuli hiyo muhimu ya Qur'ani ni kuwahamasisha vijana wazingatie mafundisho ya Kiislamu na kutekeleza majukumu yao ya kidini.
Benki ya Kiislamu ya Dubai iliasisiwa mwaka 1975 na ni moja ya wadhamini wakubwa wa mashindano ya Qur'ani ya Ras al Khaimah. 752127
captcha