IQNA

Matumaini ya kurejea Imam Musa Sadr

14:33 - February 23, 2011
Habari ID: 2085387
Vyama vya kisiasa nchini Lebanon vimelaani ukatili uanaofanywa na utawala wa dikteta Muammar Gaddafi dhidi ya wananchi na kuelezea matumaini kuwa hatima ya Imam Musa Sadr itajulikana baada ya utawala huo kuangushwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la Beirut, aghalabu ya vyama vya kisiasa nchini Lebanon vinawaunga mkono wananchi wa Libya na kuelezea matumaini kuwa watapata ushindi katika harakati zao dhidi ya dikteta Gaddafi. Wanasiasa wa Lebanon wanasema serikali mpya itakayokuja madarakani nchini Libya inapaswa kuborosha uhusiano na Beirut na Tripoli kwa kuweka wazi hatima ya Imam Musa Sadr, mwanazuoni mwandamizi wa Kishia na mwanzilishi wa harakati ya Amal ya Lebanon, ambaye alitoweka baada ya kukutana na Gaddafi nchini Libya Agosti mwaka 1978. Uhusiano na Libya na Lebanon uliharibika tokea wakati huo.
Katika taarifa, chama cha Hizbullah cha Lebanon kimeunga mkono harakati ya wananchi wa Libya ya kuwakomboa wananchi na Sayyid Sadr kutoka kwenye utawala wa kigaidi wa Gaddafi. Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu wenye kutetea uhuru hawawezi kunyamazia kimya ukatili unaofanywa na utawala wa Gaddafi katika miji ya Libya. 751850
captcha