IQNA

Madrasa ya Qur'ani yaanzishwa Somalia

14:37 - February 23, 2011
Habari ID: 2085428
Madrasa ya kwanza ya Qur'ani imeanzishwa katika mji wa Burama nchini Somalia kwa hima ya Taasisi ya Masuala ya Kheri ya nchi hiyo.
Sherehe ya ufunguzi wa madrasa hiyo ya Qur'ani imehudhuriwa na maulamaa wa Kiislamu, wahadhiri wa vyuo vikuu, maafisa wa Wizara ya Elimu, waandishi habari na wawakilishi wa Taasisi ya Masuala ya Kheri ya Kiislamu.
Sherehe hiyo imehutubiwa na Mufti mkongwe wa eneo la Odal Sheikh Abdullah Ali Jouhar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Masuala ya Kheri ya Kiislamu Siddiqi Mahmoud ambao wamesisitiza juu ya umuhimu wa madrasa za Qur'ani na kutolewa elimu ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu kwa vijana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kheri ya Kiislamu amesisitiza kuwa imepangwa kuwa madrasa kadhaa za Qur'ani zitaanzishwa katika maeneo mbalimbali ya Somalia katika miaka ijayo. 751846
captcha