Kwa mujibu wa tovuti ya thepeninsulaqatar nuskha hizo za Qur'ani zitaonyeshwa na kuuzwa katika hoteli ya Ritz Carlton mjini Doha.
Mbali na nuskha hizo za Qur'ani, baadhi ya bidhaa za sanaa kama vile kaligrafia, mapambo ya dhahabu, sanaa za mikono za zama za watawala wa Safawi na Wamoghli pia zitauzwa.
Moja ya nuskha hizo ni ile iliyopambwa kwa maji ya dhahabu ambayo inafungamana na milenia ya kumi au kumi na moja Hijiria ambayo iliandikwa kwa hati ya kufi nchini Iran.
Baada ya Doha mnada wa nuskha hizo za Qur'ani na athari za sanaa utafanyika tarehe 8 Machi mjini London. 752621