Duru ya 62 ya masomo ya maimamu wa misikiti na wahubiri wa Kiislamu ambayo ilianza tarehe 12 Februari katika Chuo Kikuu cha Shaghra mjini Riyadh, Saudi Arabia ilimalizaka jana Jumatano tarehe 23 Februari.
Kwa mujibu wa tovuti ya alriyadh, masomo hayo yamedhaminiwa na Taasisi Kuu ya Maimamu wa Misikiti na Wahubiri ya Chuo Kikuu cha Tayyiba kwa ushrikiano wa Chuo Kikuu cha Shaghra.
Masomo hayo ambayo yamefanyika kwa shabaha ya kunyanyua kiwango cha mwamko na ujuzi wa maimamu na wahubiri wa Kiislamu yamejumuisha mbinu na njia mbalimbali za kuwawezesha maimamu na wahubiri kukabiliana na masuala mbalimbali yanayojitokeza katika nyanja za shughuli zao.
Vikao vya hotuba na warsha za masomo ni baadhi ya ratiba za pembeni zilizotekelezwa kwenye masomo hayo. 752553