IQNA

Televisheni ya satalaiti ya Ahlul Qur'an kufunguliwa rasmi karibuni

15:25 - February 26, 2011
Habari ID: 2086409
Nabil Abdul Aziz al-Hammad mkuu wa kanali ya satalaiti ya Ahlul Qur'an ambayo inafungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdh al-Qur'an ametanagaza habari ya kufunguliwa rasmi hivi karibuni televisheni hiyo ya satalaiti.
Al-Hammad amesema kuwa kanali hiyo ya televisheni itafunguliwa rasmi na Abdul Aziz Khoja, Waziri wa Masuala ya Utamaduni na Habari wa Saudi Arabia na Abdallah bin Abdul Muhsin at-Turki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu.
Matangazo ya majaribio ya kanali hiyo ambayo itakuwa ikitangaza shughuli na mashindano ya Qur'ani kutoka pembe zote za dunia yamekuwa yakirushwa hewani tokea mwezi wa Ramadhani uliopita. Al-Hammad amesema kuwa hivi sasa vipindi vya mafunzo ya usomaji Qur'ani vimewavutia watazamaji wengi duniani. 753623
captcha