IQNA

Kozi ya kusoma Qur'ani Australia

15:16 - February 27, 2011
Habari ID: 2086798
Kozi ya msingi ya qiraa ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanaume inafanyika nchini Australia kwa himaya ya Akademia ya Sayansi na Utafiti wa Kiislamu Australia ISRA.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kozi hiyo inafanyika kwa lengo la kutoa mafunzo kuhusu mbinu za kusoma Qur'ani kwa Waislamu wa Australia na kuwahimiza kusoma kitabu hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu. Kozi hiyo inayofanyika katika makao ya Akademia ya Kisayansi na Utafiti wa Kiislamu Australia itakuwa ikifanyika siku ya Jumapili kila wiki na washiriki watajifunza tajweed na mbinu za qiraa.
Inatazamiwa kuwa baada ya kozi, washiriki ambao aghalabu ni wazungumuzaji wa lugha ya Kiingereza wataweza kusoma Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiarabu na kwa kuzingatia misingi ya tajwidi. Kozi hii iliyoanza mwzi Februari 15 itaendelea kwa muda wa wiki 12. 753873
captcha