IQNA

Mashindano ya Qur'ani na Hadithi kufanyika Saudi Arabia

12:09 - March 03, 2011
Habari ID: 2089587
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) yaliyopewa jina la Muhammad bin Jalwi yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 Machi katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
Akizungumzia suala hilo, Ahmad bin Hamad Albou Ali, Katibu Mkuu wa Kamati inayosimamia mashindano hayo amesema kwamba mashindano hayo yatafanyika katika hatua tatu za hifdhi ya Qur'ani Tukufu, Hadithi za Mtume na uhubiri wa dini tukufu ya Kiislamu.
Amesema sehemu nyingine ya mashindano hayo itawahusisha wafungwa wa jela za umma na pia jamii za wachache wanaoishi Saudia.
Albou Ali ameongeza kuwa usajili wa majina uliotimia kupitia mtandao wa intaneti tayari umewasajili watu 723 walio tayari kushiriki katika mashindano hayo mbali na wafungwa 120 na vilevile watu 83 kutoka jamii za wachache.
Amesema mashindano hayo yameandaliwa kwa madhumuni ya kuihudumia jamii ya Kiislamu. 756647
captcha