IQNA

Kiongozi wa Mashia wa Bahrain alaani ukandamizaji dhidi waandamanaji

21:21 - March 05, 2011
Habari ID: 2090609
Kiongozi wa Mashia wa Bahrain Ayatullah Issa Ahmad Qasim amelaani utumiaji mabavu wa askari usalama katika kuwakandamiza waandamanaji na mikusanyiko inayofanyika kwa amani.
Ayatullah Issa Qasim ambaye alikuwa akihutubia swala ya Ijumaa amelaani utumiaji mabavu dhidi waandamanaji wanaopinga serikali ya Manama na kutaja hujuma hiyo kuwa ni ya kinyama.
Amewataka viongozi wa serikali ya Bahrain kuchukua hatua halisi za marekebisho na kutahadharisha kwamba upuuzaji wa suala hilo utakuwa na matokeo mabaya.
Ayatullah Sheikh Issa Qasim amesisitiza pia juu ya udharura wa kubuniwa katiba mpya itakayodhamini matakwa ya wananchi.
Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain ametaka pia kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa na kushughulikiwa masuala ya ufisadi katika jamii. 757699



captcha