IQNA

Maonyesho ya kimataifa ya watumiaji Waislamu kufanyika Malaysia

21:33 - March 05, 2011
Habari ID: 2090610
Maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya watumiaji Waislamu yanayolenga kuarifisha mahitaji ya Waislamu yatafanyika tarehe 8 hadi 10 Mach katia mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Maonyesho hayo yatajumuisha vyakula, mavazi, vyombo vya majumbani, mapambo, vitabu, majarida na magazeti, filamu za mafunzo na za kidini na huduma za kibenki na kifedha za Kiislamu.
Maonyesho hayo yatafanyika kwa sabaha ya kuonyesha bidhaa halali za Kiislamu kwa jamii ya Waislamu milioni 15 ya Malaysia na Waislamu wa maeneo mengine duniani. Vilevile yatakuwa fursa ya kuuza bidhaa mpya, kutafuta masoko, kuarifisha makampuni mbalimbali ya uzalishaji na huduma zao na kutathmini matakwa ya watumiaji Waislamu.
Maonyesho hayo yatafanyika kwa simamizi wa Taasisi ya Kimataifa ya Asif. 757899

captcha