IQNA

Thailand kuchunguza kupigwa marufuku Hijabu

18:21 - March 06, 2011
Habari ID: 2090692
Wizara ya Elimu Thailand imesema itachunguza hatua ya wanafunzi Waislamu kunyimwa ruhusa ya kuvaa hijabu katika shule moja ya mji mkuu wa nchi hiyo Bangkok.
Wanafunzi 17 wa shule ya Wat Nongchok mwezi Oktoba waliomba ruhusa ya kuvaa hijabu ombi ambalo liliwasilishwa mbele ya Tume ya Elimu ya Msingi. Tume hiyo ilipinga ombo hilo.
Jumuiya ya Waislamu wanaotetea amani inayowakilisha wanafunzi hao iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya dini. Kamati hiyo iliamua kupeleka suala hilo katika Baraza Kuu la Sangha ambalo liliamua kuwa Hijabu iendelee kupigwa marufuku.
Uamuzi huo ulizua mjadala mkubwa kuhusu haki ya wanafunzi wa kike ya kuvaa kwa mujibu wa itikadi zao za kidini.
Waislamu nchini Thailand wanasema ni haki yao kuvaa hijabu kama ambavyo wafuasi wa dini nyinginezo walivyo na uhuru wa mavazi nchini humo.
Wizara ya Elimu Thailand inasema kimsingi haipingi vazi la hijabu. 758046
captcha