IQNA

Kongamano la Kimataifa la Quds Tukufu laanza Khartoum Sudan

18:13 - March 06, 2011
Habari ID: 2090694
Kongamano la Kimataifa la Quds limeanza leo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Sudan, Taasisi ya Kimataifa ya Baytul Muqddas imetangaza kuwa, katika kongamano hilo la siku mbili washiriki wanatarajiwa kupendekeza njia za kukabiliana na njama za Wazayuni za kuuyahudisha mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na shakhisia, wasomi na wanazuoni mbalimbali.
Sheikh Yusuf Qardhawi, Mkuu wa Muungano wa Maulama wa Kiislamu Duniani anatarajiwa kuhutubia kikao cha ufunguzi wa kongamano hilo.
Mkutano huo unafanyika katika hali ambayo asasi na taasisi mbalimbali za Palestina zimekuwa zikitahadharisha kila leo kuhusiana na kuongezeka njama za Wazayuni za kuuyahudisha mji wa Quds ambazo zinafanyika katika fremu ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.
758098
captcha