IQNA

Nuskha ya Qur'ani ya miaka 1000 China kulindwa

18:01 - March 06, 2011
Habari ID: 2090695
Nuskha ya maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu yenye umri wa miaka 1000 iliyopatikana mkoani Shandong mwaka 2008 sasa inasubiri msaada wa serikali ya China kwa ajili ya kutayarishiwa jumba maalumu la makumbusho mahala itakapohifadhiwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Arabic.peopledaily, bunge la eneo la Shandong kaskazini magharibi mwa China limeiomba serikali kuu itoe idhini ya kujengwa jumba maalumu la makumbusho ili kuhifadhi msahafu huo wa kale.
Mwa Wan Bi Naibu Mkuu wa Kongamano la Ushauri la Sera za Watu wa China amesema kuwa: “Waislamu wa mkoa wa Shandong pia wametoa ombi la ujenzi wa jumba la makumbusho kuhifadhi nuska hiyo ya Qur'ani”.
Nuskha hiyo ya Qur'an ambayo inaaminika kuwa ya kale zaidi nchini China iliandikwa kwa mkono katika karne ya 8 au 9 Miladia.
Kwa mujibu wa gazeti la People's Daily la China, wataalamu wanasema Qur'ani hiyo iliingizwa China kutoka Asia ya Kati.
Kutokana na muundo wa jalada lake, nakshi, muundo wa kaligrafia na karatasi, Qur'ani hiyo inahesabiwa kuwa moja ya nuskha za kale zaidi za Qur'ani Tukufu duniani.
758084
captcha