IQNA

Walimu wa taasisi za Qur'ani wakutana Karbala

18:25 - March 06, 2011
Habari ID: 2091228
Walimu wa vituo na taasisi za Qur'ani kutoka miji tofauti ya Iraq wamekutana katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya kujadili njia za kutatua matatizo yaliyopo kuhusiana na njia za kufundisha kitabu hicho kitakatifu.
Agenda hasa ya kikao hicho kilichofanyika katika Haramu ya Imam Hussein (as) ilikuwa ni kujadili njia za kuboresha na kukamilisha mpango muhimu wa Milenia ya Qur'ani Tukufu katika muda ulioainishwa.
Washiriki wa kikao hicho walisisitiza juu ya umuhimu wa kutolewa mafunzo maalumu ya kuboresha viwango vya elimu ya walimu pamoja na kuimarisha uelewa wao kuhusiana na masuala mbalimbali yanayojiri ulimwenguni.
Washiriki pia walifahamishwa kwamba hivi sasa taasisi ya Qur'ani ya Dar al-Qur'ani Karim inatumia mbinu za kisasa kabisa katika mafunzo ya Qur'ani.
Mahfali ya Qur'ani pia ilifanyika pembeni ya kikao hicho ambapo wasomaji Qur'ani mashuhuri wa Iraq na wafanyaziara wa Haram ya Imam Hussein (as) walipata fursa ya kunufaika nayo. 758693
captcha