Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, aliyetenda kitenco cha kuichoma moto Qurani ni Handa Tuma Mkazi wa Unguja. Hukumu ya adhabu ilitolewa na hakimu Khamis Ali Simai wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, baada ya kumtia hatiani.
Akifafanua adhabu hizo hakimu Khamis alisema shitaka la kwanza la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani atalipa faini ya Sh200,000 na endapo atashindwa atatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi sita.
Kuhusu shitaka la kuivunjia heshima dini, mahakama hiyo imempa adhabu ya kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi 18, na kufahamisha kuwa adhabu zote hizo zitakwenda sambamba.
Alisema pamoja na hilo pia mtuhumiwa huyo ambaye alipatikana na makosa hayo alipewa adhabu mbili hizo ili iwe fundisho kwa wengine kutofanya makosa kama hayo. Zanzibar ni eneo la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lenye mamlaka ya ndani. Asilimia 99 ya wakaazi karibu milioni moja wa Zanzibar ni Waislamu.
Kwa mujibu wa mahakama hiyo, Ramadhan Handa Tuma alifanya kitendo Novemba 16, mwaka jana hadharani kwa makusudi na bila ya halali alichoma moto Qurani kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii ya kiislamu Zanzibar.
758479