Mahand Khorshid ametoa matamshi hayo katika Kongamano la 24 la Umoja wa Kiislamu lililofanyika hivi karibuni mjini Tehran.
Akizungumza na IQNA, amesema wimbi la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo katika nchi za Magharibi ni jambo ambalo limewafanya wengi watake kuujua Uislamu.
Akiashiria umuhimu wa ukuruba wa madhehebu ya Kiislamu amesema kuwa, 'dini ni suala la kimsingi miongoni mwa vijana na kuna haja ya kuwafanya waifahamu dini ya Kiislamu kikamilifu'. Aidha amewataka vijana kuchukua tahadhari kuhusu madhehebu potofu yanayoibuka.
Msomi huyo wa Ujerumani ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa kongamano la kimataifa la Umoja wa Kiislamu.
Kongamano hilo la kila mwaka lilifanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Februari 19.
759333