IQNA

Kikao cha Qur'ani kufanyika Kuwait

15:45 - March 07, 2011
Habari ID: 2091937
Kikao kuhusu mafundisho ya Qur'ani Tukufu kitafanyika nchini Kuwait kuanzia Machi 28-30, ametangaza mkuu wa masuala ya Qur'ani na Taaluma za Kiislamu katika Wizara ya Awqaf nchini Kuwait.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Ra'y Abdullah Mahdi Barak amesema kikao hicho kinalenga kuchunguza nafasi ya Qur'ani katika sekta ya elimu.
Amesema kikao hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Al Seraj al Munir chini ya kaulimbiu ya "kuelekea kwenye mafundisho bora ya Qur'ani".
"Kustawisha harakati za Qurani, kubainisha nafasi ya Qur'ani katika uga wa elimu, kustawisha utamaduni wa familia katika masuala ya elimu na mafundisho ya kidini na kubadilishana mawazo taasisi za kitaifa na kimataifa ni kati ya malengo ya kikao hicho", imesema taarifa ya Wizara ya Awqaf.
759234
captcha