Chuo hicho kitaanzishwa na shirika la Wealth Management Pvt. Ltd lenye makao yake Mumbai India. Shirika hilo ambalo hutoa muongozo kuhusu kusimamia utajiri kwa mujibu wa sheria za Kiislamu limesema chuo hicho kinawahimiza vijana kujisajili katika kozi zake ili waweze kupata ajira na kufanya biashara katika sekta ya fedha yenye idadi ndogo ya Waislamu hivi sasa.
Mkurugenzi wa Pragmatic Wealth Management Pvt. Ltd Dkt. M Y Khan amesema kuna haja ya kuwepo na wataalamu Waislamu katika taasisi za kifedha na benki za Kiislamu.
759392