Hujjatul Islam wal Muslimin Tawfiq al A'amir amekuwa akishikiliwa na polisi katika mji wa Damam kwa muda wa wiki moja. Punde baada ya kuachiliwa huru ameonana na Mohammad bin Fahd Mkuu wa eneo la Mashariki mwa Saudi Arabia ambalo wakaazi wake wengi ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Katika mkutano huo Hujjatul Islam wal Muslimin al A'amir amemfahamisha afisa huyo matakwa ya Mashia. Amebainisha wazi kuhusu hali ya Mashia katika eneo la Al Ahsaa. Aidha ametaka waachiliwe huru watu tisa waliotiwa mbaroni mwaka 1996 kwa tuhuma za kulipua kituo cha kijeshi cha Marekani cha Khobar nchini Saudia ambapo Wamarekani 19 waliuawa.
Mohammad bin Fahd Mkuu wa eneo la Mashariki mwa Saudi Arabia amesema matakwa ya Mashia yatajadiliwa katika kikao kitakachohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa eneo hilo.
Hujjatul Islam wal Muslimin al A'amir alitiwa mbaroni baada ya kutoa hotuba katika Msikiti wa Aimaa al Baqiee AS huko Al Ahsaa ambapo alitaka utawala wa ufalme wa kikatiba uanzishwe Saudi Arabia badala ya ufalme wa sasa wa kiimla.
759402