IQNA

Qur'ani kunawiri katika Mashariki ya Kati mpya

14:19 - March 08, 2011
Habari ID: 2092113
Mwamko katika Mashariki ya Kati umepelekea eneo hili kuwa uga mpya wa kufikia malengo ya juu ya Qur'ani na Uislamu.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Dawati Mkuu wa Masuala ya Qurani katika Taasisi ya Wanachuo Wairani ya Harakati za Qurani. Akizungumza na IQNA, amesema kuwa: "Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu maadui wote wa Uislamu walielekeza propaganda zao dhidi ya Iran lakini walifeli kufikia malengo yao".
Ameongeza kuwa kadiri wanavyotumia propaganda chafu dhidi ya Uislamu ndivyo wanavyoshindwa kufikia malengo yao haramu.
Hujjatul Islam Dawati ametoa wito kwa vyombo vya habari vya Kiislamu kujizatiti kwa teknolojia za kisasa ili kukabiliana na hujuma ya propaganda za maadui.
759248
captcha