IQNA

Kikao cha kimataifa cha sira ya Mtume (saw) chafanyika Pakistan

13:55 - March 08, 2011
Habari ID: 2092222
Kikao cha kimataifa cha sira ya Mtume Mtukufu (saw) kilianza jana Jumatatu tarehe 7 Machi huko Islamabad mji mkuu wa Pakistan.
Kwa mujibu wa tovuti ya The News kikao hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Sauti ya Kiislamu ya Pakistan kwa madhumuni ya kuarifisha pande tofauti za maisha ya Mtume (saw) na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa msingi wa mafundisho ya mtukufu huyo.
Kueneza amani, maelewano, kuvumiliana na kuishi pamoja kwa amani watu wa jamii mbalimbali kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume (saw) ni malengo mengine ya kufanyika kikao hicho cha kimataifa.
Wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka nchi 15 za dunia wanashiriki katika kikao hicho cha siku tatu ambapo wanatoa hotuba kuhusiana na masuala tofauti yaliyoainishwa katika ajenda ya kikao hicho. 759142
captcha