IQNA

Kongamano la Muujiza wa Qur'ani lafanyika Karbala

22:19 - March 08, 2011
Habari ID: 2092751
Kongamano la kielimu la Muujiza wa Qur'ani Tukufu, Sayansi na Elimu nafsi lilifanyika jana katika Chuo Kikuu cha Karbala.
Muhammad Shahab Ahmad, msomi wa sayansi ya Qur'ani wa Iraq na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Karbala alihutubia kongamano hilo kuhusu muujiza wa Qur'ani na elimu nafsi.
Muhammad Shahab Ahmad ambaye ameshiriki kwenye kongamano hilo kwa ombi la Chuo Kikuu cha Karbala ametoa ufafanuzi kuhusu muujiza wa kisayansi wa Qur'ani Tukufu na uhusiano wake na elimu nafsi.
Muhammad Shahab Ahmad ni mtaalamu wa maudhui ya muujiza wa Qur'ani na hadi sasa amekwisha hutubia mikutano mingi ya kimataifa akizungumzia mada hiyo. 759946
captcha