Kituo cha habari cha Wizara ya Hija ya Saudi Arabia kimeripoti kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Sultan bin Abdul Aziz ndiye atakayesimamia mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Masuala ya Kidini ya jeshi la Saudia Abdullah bin Saleh bin Abdul Hamid Al al Sheikh amesema karibu washindani 90 kutoka nchi 20 za Kiarabu na Kiislamu wanashiriki katika mashindano hayo.
Mashindano ya kimataifa ya majeshi yatafanyika katika nyanja nne za kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na tartili na tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 na tartili na tajwid, hifdhi ya juzuu 10 na tartili na tajwidi na hifdhi ya juzuu tano za Qur'ani Tukufu.
Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani ya wanajeshi yalifanyika mwaka 2001 nchini Saudi Arabia. 760007