IQNA

Arbaini ya Ayatullah Muhammad Ali al-Amri kufanyika

14:23 - March 09, 2011
Habari ID: 2093225
Arbaini ya Ayatullah Sheikh Muhammad Ali al-Amri, aliyekuwa kiongozi wa kimaanawi wa Mashia wa mji mtakatifu wa Madina nchini Saudi Arabia itafanyika hapo kesho Alkhamisi tarehe 10 Machi.
Katika maombolezo hayo filamu fupi ya maisha ya mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kishia itaonyeshwa na pia waombolezaji kugawiwa cd za filamu hiyo ya kweli. Filamu hiyo inajumuisha maisha yake ya ujana akiwa masomoni na pia hotuba zake alizotoa katika vipindi tofauti vya maisha yake yenye mabaraka kubwa.
Ayatullah al-Amri aliaga dunia Jumatatu tarehe 24 Januari baada ya kuhudumia dini kwa miaka 60. Mazishi yake yalikuwa makubwa ambapo waombolezaji kutoka nchi tofauti za dunia walishiriki.
Shakhsia na viongozi tofauti wa Kiislamu walituma salama zao za rambirambi kufuatia kifo cha mwanazuoni huyo aliyepata mateso makubwa kutoka kwa utawala wa Kiwahhabi wa Saudi Arabia. 760209

captcha