Umar al Fariq alikuwa miongoni mwa wafasiri wa Qur'ani na tafsiri yake imepata umashuhuri mkubwa kati ya Waislamu wa Somalia na nchi nyingine za Kiafrika.
Alizaliwa mwaka 1940 katika moja ya vijiji vya magharibi mwa Somalia katika familia ya kidini na mama pamoja na baba yake ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni maarufu wa Kiislamu akiwa na umri wa miaka 6.
Alihifadi Qur'ani nzima akiwa na umri wa miaka 12 na alianza kufunza Qur'ani kwa watoto wadogo miaka miwili baada ya kuhifadhi Qur'ani nzima.
Umar al Faruq alipata elimu ya msingi katika kituo cha elimu cha al Tadhamun al Islami mjini Mogadishu na alikamilisha elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Madina.
Athari muhimu zaidi ya msomi huyo wa Kiislamu ni tafsiri yake ya Qur'ani ambayo aliiandika alipokuwa katika nchi za Magharibi alikokwenda kueneza mafundisho ya dini ya Kiislamu. 760696