Amesema Nigeria itanufaika na mafanikio ya Malaysia katika kufikia lengo hilo. Amesema Nigeria ina nafasi muhimu katika Baraza la Huduma za Kifedha za Kiislamu na kwamba iko mbioni kuimarisha shughuli za mfumo wa benki za Kiislamu nchini.
Lamido Sanusi amesema wataalamu wengi wa masuala ya kifedha wanaamini kwamba nchi za Asia za Malaysia na Indonesia zinashuhudia ustawi mkubwa katika nyanja mbalimbali za kifedha na kiuchumi kutokana na kutekeleza mfumo wa kifedha wa Kiislamu katika hali ambayo nchi nyingi za Ghuba ya Uajemi zimekuwa na ustawi wa kadri katika uwanja huo.
Waislamu wa Nigeria wanaunda zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo ambayo ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Afrika. 761127