IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Mazungumzo kati ya Uislamu na Japan' chamalizika Imarati

17:56 - March 10, 2011
Habari ID: 2093510
Duru ya tisa ya vikao vya Mazungumzo kati ya Uislamu na Japan ambayo ilianza hapo siku ya Jumatatu huko Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu ilimalizka siku ya Jumanne Machi 8.
Washiriki wa kikao hicho walitoa taarifa mwishoni mwa kikao chao na kusisitiza juu ya udharura wa kufanyika mazungumzo ya staarabu mbalimbali, utatuzi wa changamoto za zama na utatuliwaji wa matatizo yanayowakabili vijana. Washiriki pia walisisitiza umuhimu wa kuimarishwa ushirikiano wa kiutamaduni, kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Kiislamu na Japan na kusema kuwa jambo hilo ni muhimu sana katika kudhamini mahitaji ya vizazi vijavyo. Vikao hivyo vilianza kufanyika mwaka 2001 wakati wa uongozi wa Yohei Kono, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan na hadi sasa tayari duru nane za vikao hivyo zimefanyika katika nchi za Bahrain, Tunisia, Saudi Arabia, Iran, Kuwait na Japan. Kujadiliwa masuala ya kunufaika na teknolojia ya kisasa katika kuimarisha uchumi wa nchi husika kwa manufaa ya vizazi vijavya ni lengo kuu la kufanyika vikao hivyo. 761070
captcha