Hayo yamesemwa na Daktari Ali Akbar Momen katibu wa 'Kongamano la Qurani na Afya' lililofanyika Machi 9 katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Jondi Shapoor katika mji wa Ahvaz kusini mwa Iran.
Qurani Tukufu imetilia mkazo saana suala la afya, amesema, na kutoa wito wa kuzingatiwa suala la afya kwa mujibu wa Qurani Tukufu.
Makala 58 ziliwasilishwa katika kongamano hilo. Kati ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na "Qurani na Afya ya Kisaikolojia" , "Qurani na afya ya kifisiolojia" na "Qurani na Afya ya Kijamii".
760955