Akizungumza Machi 8 mjini Tehran kwa mnasaba wa kuzinduliwa tarjumi mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kihispania, Mohammad Bagher Khorramshad ameashiria ushawishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa sasa katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema: "Kuhusu mwamko wa sasa duniani, macho yote yameelekezwa Iran kwa sababu yaliyosema na viongozi wa Iran miaka 32 iliyopita sasa yanajiri".
"Ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu utakuwa na ushawishi zaidi iwapo utaenezwa kupitia tarjumi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwani msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni Qur'ani".
Tarjumi hiyo mpya ya Qur'ani ya Kihispania imechapishwa na Kituo cha Tartjumi na Uenezi wa Mafundisho ya Kiislamu kwa ushirikiano na Taasisi ya Andishe-ye-Sharq.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tarjumi hiyo ilizinduliwa katika sherehe zilizohudhuriwa na Bw. Mohammad Baqer Khorramshad Mkuu wa ICRO na Hujjatul Islam Rabbani Mkurugenzi wa Taasisi ya Andishe-ye-Sharq, mtarjumi, wataalamu wa utamaduni na wataalamu na wanafunzi wa lugha ya Kihispania.
760441