IQNA

Benki ya kwanza ya Kiislamu yaanzishwa Maldives

12:58 - March 10, 2011
Habari ID: 2093540
Benki ya kwanza ya Kiislamu imefunguliwa nchini Maldives katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais wa nchi hiyo Mohammad Nasheed.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Maldives Harith Harun amesema benki hiyo imezinduliwa ikiwa na mtaji wa dola milioni 12. Amesema banki hiyo itakuwa na aina kadhaa ya akaunti ambazo hazitakuwa na riba.
Amesema banki hiyo pia itatoa mikopo kwa watu binafsi na mashirika ya kibiashara kwa mujibu wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu wa Murabaha, Ijara na Musharakah.
Mfumo wa benki za Kiislamu umekuwa ukienea kwa kasi kubwa kote duniani kutokana na walimwengu kuchoshwa na mfumo wa riba ambao umegeuka na kuwa jinamizi.
Itakumbukwa kuwa katika mgogoro wa uchumi duniani ambapo benki nyingi zilisambaratika, benki za Kiislamu zilibakia imara na hivyo kuwavutia wateja wengi wakiwemo Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
760367

captcha