IQNA

Mwanafunzi Syria ahifadhi Qurani nzima kwa siku 75

16:27 - March 12, 2011
Habari ID: 2093805
Mwanafunzi wa shule moja nchini Syria amefanikiwa kuhifadhi Qurani nzima kwa muda wa siku 75.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Damascus, mwanafunzi huyo wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Sharia ya mji wa Aleppo kijijini Torkman Barhameweka rekodi kwa kuhifadhi Qurani nzima katika kipindi kifupi.
Akiwa chini ya muongozo wa mwalimu wake mwanafunzi huiyo alikuwa akihifadhi kurasa 10 za Qurani kila siku katika kipindi cha miezi miwili na nusu.
Mwanafunzi huyo alienziwa katika sherehe iliyofanyika katika Shule ya Shariat wiki jana.
761586

captcha