Mashindano ya mchujo yalifanyika Febrari 23 na yalijumuisha pia mashindano ya sera ya Mtume SAW.
Kwa mujibu wa Murtadha Mahmoudi Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika tawi la Tehran la chuo hicho, mashindano ya maandishi ya Qur'ani yatafanyika katika eneo la Rey mjini Tehran.
Ameongeza kuwa mashindano ya Qur'ani yatafanyika katika matawi yote ya chuo hicho kote Iran wakati mmoja na washindi kutangazwa mwaka mpya Hijria Shamsia (1390)
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad kina wanafunzi milioni moja na nusu na kinahesabiwa kuwa chuo cha tatu kwa ukubwa duniani. Chuo hicho kina matawi 400 kote Iran na nchi kadhaa duniani kama vile Uingereza na Imarati.
761813