Katibu wa Mashindano ya 13 ya Taifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Saudi Arabia Mansur bin Muhammad amesema mafunzo hayo ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya majaji wa Qur'ani yatafanyika yapata miezi mitatu ijayo kwa usimamizi wa Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo.
Ameongeza kuwa lengo la kutolewa mafunzo hayo ni kutayarisha majaji wa Qur'ani na kunyanyua ujuzi na maarifa yao kwa ajili ya mashindano ya kieneo na kimataifa.
Mansur bin Muhammad amesema masomo hayo yatahusu pande mbili za kinadharia na kivitendo. 762630