IQNA

Mashindano ya Qur'ani Brunei

15:13 - March 14, 2011
Habari ID: 2095754
Robo fainali ya mashindano ya kitaifa ya qiraa ya Qur'ani kwa ajili ya watu wazima yanaendelea nchini Brunei katika Msikiti wa Setia Ali mjini Muara.
Mashindano hayo ya siku nne yalianza Jumamosi na yanajumuisha washiriki 85.
Hafla ya kutoa zawadi kwa washindi itafanyika Jumanne alasiri.
Washiriki 20 wa kike na kiume watakaofuzu watashindana katika nusu fainali baadaye.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Masuala ya Kidini nchini humo kwa lengo la kuhimiza na kuimarisha kiwango cha qiraa mbali na kuwahimiza Waislamu nchini humo kusoma Qur'ani.
763370
captcha