IQNA

Hizbullah yalaani ukandamizaji dhidi ya wapinzani Bahrain

9:06 - March 15, 2011
Habari ID: 2096045
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikilaani ukandamizaji unaofanywa na askari usalama wa utawala wa Bahrain dhidi ya wananchi wanaoandamana kupinga utawala wa kifalme nchini humo.
Taarifa hiyo imesema kuwa utumiaji huo wa mabavu na nguvu ziada dhidi ya wananchi wanaofanya maandamano ya amani wakidai haki zao za kisiasa ulianza muda mfupi baada ya safari ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates mjini Manama.
Hizbullah imesema inalaani hatua hiyo inayofanyika dhidi ya wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Bahrain na kwamba ni ukiukaji wa haki ya kujieleza na haki za kimsingi za wananchi wanaotaka kushirikishwa katika masuala muhimu ya nchi yao. Imesisitiza kuwa haki hizo zimedhaminiwa katika dini na sheria zote za kimataifa.
Taarifa ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeongeza kuwa utumiaji nguvu kupita kiasi dhidi ya wananchi hautakuwa na maslahi kwa mustakbali wa Bahrain, na kinyume chake utakuwa na taathira hasi kwa amani na utulivu wa nchi hiyo. Imesema, ukandamizaji huo utakwamisha juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa sasa wa Bahrain. 763503


captcha