Kituo cha habari cha Palestine Info kimeripoti kuwa walowezi wa Kizayuni walivunjia heshima uwanja wa ndani wa msikiti mtakatifu wa al Aqsa na kuanza kuwachochea watu waliokuwa wakiekeleza ibada ya swala katika eneo hilo. Muda mfupi baadaye askari wa utawala ghasibu wa Israel waliwashambulia Waislamu waliokuwa wakiswali na kumjeruhi mmoja wao. Askari hao pia wamewatia nguvuni Wapalestina wengine watatu.
Ripoti zinasema kuwa baada ya machafuko hayo askari zaidi wa Israel walitumwa katika uwanja wa msikiti wa al Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu wote duniani. 763798