Kwa mujibu wa tovuti ya Palestin Info, jumuiya hiyo imesema kuwa Ukanda wa Gaza pia unahitajia sana shule ambazo zitaondoa mgogoro wa elimu na masomo katika ukanda huo.
Kwa mujibu waripoti hiyo wakazi wa baadhi ya maeneo ya ukanda huo hupata maji mara moja tu kwa siku katika hali ambayo maeneo mengine mengi hupata maji mara moja kila baada ya siku tatu. Pia imesema kuwa wakazi wa ukanda huo hukatiwa umeme kati ya masaa manne hadi sita kila siku jambo linalotatiza sana shughuli zao za kila siku.
OIC imesema ili kupunguza mgogoro wa masomo katika ukanda huo, kwa uchache shule na taasisi za elimu 30 zinapaswa kujengwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo. OIC imeendelea kusema kuwa vikwazo na mzingiro unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika ukanda huo umewasababishia matatizo zaidi Wapalestina kwa kuzuia wagonjwa wanaoteseka katika ukanda huo watafute matibabu nje ya eneo hilo.
Hata Wapalestina wanaobahatika kutoka nje ya ukanda huo huzuiwa na Wazayuni kurudi makwao na kulazimika kuishi kwenye mpaka wa ukanda huo kama wakimbizi. 764233