IQNA

Tarjumi mpya ya Juzuu Amma kwa Kiswahili na Kifulani

13:12 - March 16, 2011
Habari ID: 2096889
Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limechapisha tarjumi mpya ya Juzuu Amma (Juzuu ya 30 ya Qur'ani Tukufu) kwa lugha za Kiswahili na Kifulani.
Tarjumi hizo zimechapishwa na shirika la ‘Mushaf Afriqia’ la Khartoum, Sudan kwa ushirikiano wa ISESCO, Jumuiya ya Kimataifa ya Kutangaza Uislamu na Chuo Kikuu cha Kiafrika cha Kimataifa cha Sudan.
Katika tarjumi hiyo ya Juzuu Amma maandishi ya Kiarabu yemetumika kuandika lugha za Kiswahili na Kifulani. Tarjumi hizo ni katika mpango wa ISESCO wa kuandika lugha za Waislamu Afrika kwa maandishi ya Kiarabu.
764086
captcha