IQNA

Iran yatayarisha orodha ya misahafu za kale

13:11 - March 16, 2011
Habari ID: 2096904
Maktaba na Makavazi ya Kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza mpango wa kutayarisha orodha ya misahafu za kale 1100.
Mkurugenzi wa kitengo cha nyaraka za kale katika Maktaba ya Makavazi ya Kitaifa Bw. Fathollah Keshavarz amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa idara yake imeharakisha mkondo wa kutayarisha orodha hiyo kwa kuwaajiri wataalamu.
Ameongeza kuwa nyaraka za kale ambazo zimehifadhiwa katika Maktaba ya Majlis ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ni 3,500 na kati yazo 1100 ni nyaraka za Qur'ani Tukufu ambazo ni za kutoka karne ya 2 hadi 13 Hijria Qamariya.
Ameendelea kusema kuwa Maktaba ya Taifa hadi sasa imetayarisha orodha ya nyaraka 14000 za kale kwa utaratibu wa alfabeti na kwamba nyaraza zilizosalia zitasajiliwa siku za usoni.
‘Maelezo kuhusu nyaraka hizo za kale pia yanapatikana katika tovuti ya intaneti ya Maktaba ya Taifa ya Iran’, amesema.
764070
captcha