Kongamano la Kiislamu la Quds lenye makao yake Amman Jordan limetoa taarifa likisema mji wa Quds Sharifu na Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa ni maeneo yanayokabiliwa na hujuma ya moja kwa moja ya utawala ghasibu wa Israel, walowezi wa Kizayuni na Mayahudi wenye misimamo mikali ambayo wanajaribu kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa kwa njia mbalimbali kwa lengo la kutekeleza ibada zao hapo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa miongoni mwa uchokozi wa hivi karibuni ni tangazo lililotolewa na utawala haramu wa Israel kuwa umetoa idhini kwa Taasisi ya Turathi ya Ukuta wa Magharibi kuendeleza ujenzi wa daraja la chuma linalounganisha Msikiti wa Al Aqsa na makao yake kwa kisingizio cha kuwawezesha Mayahudi kufika katika ‘Ukuta wa Kulia’. Daraja hilo litawezesha pia wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kuvamia Msikiti wa Al Aqsa wakati wowote ule. Taasisi ya Turathi ya Ukuta ya Magharibi ina misimamo ya kibaguzi na kufurutu mipaka dhidi ya Wapalestina.
Taarifa hiyo imesema hujuma ya Wazayuni inakuja katika wakati ambao nchi za Kiarabu ni dhaifu na hakuna Umoja na mshikamano wa Kiislamu.
764243