Kituo cha habari cha journaldujura kimeripoti kuwa moja ya kazi muhimu za jumuiya hiyo ni kuanzisha majlisi itakayojumuisha wawakilishi wa Waislamu wote nchini humo.
Mwenyekiti wa Federesheni ya Jumuiya za Kiislamu nchini Uswisi (FOIS) Hisham Midhar amesema Waislamu wamekuwa barani Ulaya kwa miaka mingi sasa na kwamba lengo la kuasisiwa jumuiya hiyo ya Kiislamu ni kutaka itambuliwe kama taasisi ya kisheria ndani ya serikali ya Uswisi.
"Tunataka kuboresha sura ya Waislamu nchini Uswisi na taasisi hii mpya inapaswa kuwa chombo cha kuhuisha amani kati ya dini mbalimbali. "Tunataka kukomesha propaganda chafu za kuwaogopesha watu kuhusu dini ya Kiislamu", amesisitiza Hisham Midhar. 763912