Usama an-Nujaifi, Spika wa Bunge la Iraq ametuma ujumbe katika mji mtakatifu wa Karbalaa kwa ajili ya kumshukuru Sheikh Abdul Mahdi Karbalai, msimamizi wa Haram ya Imam Hussein (sa).
An-Nujaifi ametuma ujumbe huo unaoongozwa na Abbas Fadhil Gambar, mkuu wa Ofisi yake ili kumshukuru Karbalai kutokana na mipango muhimu ya huduma aliyobuni na kutekeleza katika haram hiyo. Gambar amesema kuwa Haram takatifu ya Imam Hussein (as) ni nuru ya matumaini kwa kila mwananchi wa Iraq na kupongeza juhudi zinazofanyika katika haramu hiyo kwa madhumuni ya kutekeleza mipango ya huduma na kiutamaduni inayowanufaisha Wairaki wote kwa kuwaelimisha kuhusiana na mafundisho ya Ahlul Beit (as).
Katika safari yake aliyofanya hivi karibuni katika haram hiyo mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la Iraq, an-Nujaifi alikutana na kuzungumza na Karbalai kuhusiana na mipango mbalimbali ya huduma na utamaduni inayotekelezwa na haram hiyo kwa ajili ya wageni na wafanyaziara wa haram hiyo tukufu. 764518